SOKO LA BIADHAA TANZANIA (TMX) LABAINISHA FURSA KWA WAUZAJI NA WANUNUZI BIDHAA NDANI NA NJE YA NCHI

NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DAR ES SALAAM

WAUZAJI
na wanunuzi wa bidhaa ndani na nje ya nchi wamehamasishwa kutumia Soko la
Bidhaa Tanzania (TMX) ili kuongeza ufanisi katika shughuli zao, Afisa Mtendaji
Mkuu (CEO) wa TMX, Bw. Godfrey Malekano amesema.

Ameyasema
hayo jijini Dar es Salaam, Septemba 7, 2023, katika kikao kazi na wahariri na
waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari, kilichoandaliwa na TMX chini ya
uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR).

Amesema
Soko la Bidhaa Tanzania ni mfumo rasmi wa Kidijitali unaokutanisha wauzaji na wanunuzi kwa
pamoja na kufanya biashara ya mikataba ya bidhaa, inayotoa uhakika wa ubora,
ujazo na malipo na kutaja bidhaa husika kuwa ni pamoja na zile za Kilimo,
Mifugo, Madini na Nishati.

Alisema
washiriki katika Soko la Biadhaa Tanzania ni pamoja na Wauzaji Bidhaa (Vyama
vya Ushirika, AMCOS, Vikundi vya Wakulima, Wasindikaji, Wachenjuaji, Wanunuzi,
Wafanyabiashara (wauzaji wa bidhaa nje ya nchi) Wanaonunua kwa ajili ya kuuza
baadae, Wasindikaji, Mawakala wa soko.

“Kwa
kutumia Mfumo huu, Muuzaji anahakikishiwa malipo kwa wakati, Mnunuzi
anahakikishiwa upatikanaji wa bidhaa husika kwenye ubora na uzito stahiki.”
Alifafanua.

Hata
hivyo alitoa angalizo, kwa kuwa Mfumo huo unakutanisha wadau kutoka kila pembe
ya dunia, suala la ubora (standards) wa bidhaa, 
uhakika wa upatikanaji bidhaa ni mambo yanayopaswa kuzingatiwa.

“Hapa
kuna mambo mengi ya kuzingatia kuanzia namna tunavyozalisha (kulia), kuvuna, kuhifadhi
(Maghala).” Alifafanua.

Akizungumzia
faida ya Soko la Bidhaa Tanzania kwa upande wa Mkulima na Mnunuzi ni Kuimarisha
bei ya soko (Zaidi ya Shillingi billioni 248.74 zimelipwa kwa wakulima)
Upatikanaji wa taarifa za Soko (kupitia mabango ya kidijitali na simu janja)
Wakulima wako huru kuamua bei walioridhia kuuza bidhaa zao Kuongezeka kwa
ufahamu wa uzalishaji bora Uhakika wa Malipo.

Kwa
upande wa Serikali, Mfumo unasaidia Kuhamasisha kampeni ya uchumi wa viwanda,
upatikanaji wa taarifa za kuaminika, lakini pia ni njia rahisi za kukusanya
mapato kwa Halmashauri, njia rahisi wa ukusanyaji mapato ya taasisi husika, urahisi
wa usimamizi wa utoaji wa vibali husika kwa usafirishaji wa bidhaa zilizouzwa,
kusaidia upatikanaji wa Fedha za Kigeni (FOREX) kupitia bidhaa zinazouzwa nje
lakini pia kusaidia biashara ya kimataifa kwa gharama nafuu- Africa Continental
Free Trade Area (AfCFTA).

Ofisi
ya Msajili wa Hazina (TR) ndiyo yenye jukumu la kusimamia utendaji wa Mashirika
yote ya Umma na imeweka utaratibu kwa viongozi wa taasisi hizo kukutana na
wahariri na waandishi wa habari ili kuueleza umma wa Watanzania mambo ambayo
taasisi hizo zinatekeleza.

Chini
ya utaratibu huo TMX inakuwa ni taasisi ya 11 kukutana na wahariri na waandishi
wa habari nchini.

“Kwa
mantiki hiyo Ofisi ya Msajili wa Hazina ikaona umuhimu na msingi wa
kuzikutanisha taasisi za umma na umma wenyewe kupitia vyombo vya habari.”
Alisema Bw. Sabato Kosiri, Afisa Mwandamisi wa Uhusiano Ofisi ya Msajili wa
Hazina.

Alisema,
malengo sio tu kutoa elimu lakini iwe ufunguo kwa taasisi kufanya muendelezo wa
kutoa elimu kwa umma

Akifafanua
zaidi alisema, Msajili wa Hazina (TR) alielekeza mara kadhaa kwa Taasisi za
Umma kila zinapoandaa taarifa za fedha za kila mwaka wahakikishe zinatangazwa
ili umma ujue mwenendo wa Mashirika yao.

“Umma
ukiwa na uelewa wa kutosha itakuwa rahisi kwao kubaini usahihi wa kinachoelezwa
kuhusu taasisi fulani.” Alisema Sabato.

 

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) Bw. Godfrey Malekano akizungumza wakati anatoa wasilisho kuhusu utekelezaji wa majukumu ya TMX wakati wa kikao kazi na wahariri na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari, kilichoandaliwa na TMX chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR). Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Eric Mkuti.

 

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) Bw. Godfrey Malekano akizungumza wakati anatoa wasilisho kuhusu utekelezaji wa majukumu ya TMX wakati wa kikao kazi na wahariri na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari, kilichoandaliwa na TMX chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR).
Bw. Manyerere Jackton, akionegea kwa niaba ya Mwneyekitiw a Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) Bw. Godfrey Malekano akizungumza wakati anatoa wasilisho kuhusu utekelezaji wa majukumu ya TMX wakati wa kikao kazi na wahariri na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari, kilichoandaliwa na TMX chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR).

Baadhi ya maafisa wa TMX, wahari na waandishi wa habari wakimsikilzia CEO, Malekano

 

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Sabato Kosuri akitoa neno la utangulizi

 

 
 

 

Bw. Augustin Mbulumi, Meneja Uendeshaji TMX.

 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Eric Mkuti (kushoto) akibadilishana mawazo na Afisa Mtendaji Mkuu wa TMX, Bw. Godfrey Malekano. 

Scroll to Top